Thursday, February 4, 2010

NDONDI!

Floyd "Money" Mayweather Jr sasa atazipiga na mmarekani mwenzake Shane Mosley mnamo Mei mosi mwaka huu 2010 katika ukumbi wa MGM Grand huko Las Vegas California.
Mayweather na Mosley ambao waliishaanza kupigana mkwara tangu mwaka jana mara baada ya mpambano kati ya Mayweather na Juan Manuel Marquez.
Kambi za mabondia hawa wote wawili zimekubaliana na sharti ya kambi ya Mayweather la kupima damu kila wiki wakati wa maandalizi wa mpambano huo sharti ambalo lilipelekea kuvunjika kwa mpambano kati ya Mayweather na Manny Pacquiao mapema mwaka huu,kambi ya mfilipino Pacquiao ilikataa kata kata kukubaliana na sharti hilo ambalo ni staili ya michezo ya olympic.
Sasa sijui nani kati ya mabondia hawa nguli anamuhofia mwenzake?