Sunday, November 29, 2009

Kumradhi wadau siko hewani tangu juzi niko safarini,kwny mnuso na kiji-vekesheni kidogo cha thanksgiving hapa mji kasoro bahari dallas texas,kwhy msikonde wadau kaeni mkao wa kula subirini taswiraz za kumwaga.........................................

Monday, November 23, 2009

BWI tayari kurudisha mkoko wa kukodi kabla ya kukwea gari moshi kuelekea Philly,PA kumalizia vekesheni yangu ya bila malipo duh!


Club Safari with my primary school mate Rich,naye tulikuwa hatujaonana tangu tumalize elimu ya msingi enzi zileee,kumbe alitimkia "ng'ambo"


Kweli milima haikutani lkn binadamu hukutana,baada ya takriban muongo mmoja nilikutana na mdau John6(mbele)aliyejichimbia huko kwa Obama!


Nikila "mikonozzz" na my uncle,aunt na mdau wa TX,kwa Obama jumba jeupe!


Club Ozio nikiwa na wadau wa Dc Jenge & Jabir,hii club ina ghorofa kama tano hivi zinazopita muziki wa mahadhi tofauti,hapa anakamua m-bongo DJ Joe!


Mzee wa ng'ambo akiwa vekesheni fupi kwa Obama,uncle GK,mdau wa Texas mtembelee ktk (willemwamba.blogspot.com) na mdau wa Dc Jabir.Club Safari DC.


Mzee wa ng'ambo akiwa kwny mnuso wa kuzaliwa wa mdau Jimmy K(mwenye T-shirt nyekundu),DJ Evy na mdau wa Kibaigwa Joram aliyeshika beer.


Friday, November 20, 2009

Sakata la Ireland vs France!

Baada ya hapo jana shirikisho la soka la Ireland kuwasilisha rufani yao kwa Fifa kuomba mechi ya mtoano ya kufuzu kushiriki kombe la dunia 2010 huko Afrika ya Kusini irudiwe,leo Fifa imetoa majibu ambapo imekataa rufaa hiyo na kusisitiza kwamba kanuni namba tano ya shirikisho hilo isemayo uamuzi wa refa ni wa mwisho,ingawa Thierry Henry mwenyewe amekiri kwamba aliunawa mpira kwa makusudi!!!!Kweli umefika wakati wa Fifa kuruhusu matumizi ya teknolojia ya picha za televisheni kutatua matatizo kama haya ya wachezaji wadanganyifu.
Pole kwa kocha,wachezaji,mashabiki wa soka wa Ireland,timu mnayo na ilistahili kukata tiketi ya kwenda Afrika ya Kusini.