Saturday, January 22, 2011

African Stars "Twanga Pepeta" Usiku wa Mwafrika Billicans

Safu nzima ya bendi ya twanga pepeta wakilishambulia jukwaa kwa staili yao mpya ya "kusugua kisigino"ktk usiku wa mwafrika kila siku ya jtano ndani ya klabu Billicanas almaarufu kama "Bills'

Manchester United 5 Birmingham 0

Dimitar Berbatov (pichani) akifunga bao la kwanza ktk mechi kati ya Man.Utd na B'ham ktk mchezo wa ligi kuu ya uingereza.Berbatov alifunga mabao matatu ktk mchezo huo,huku mkongwe Ryan Giggs akifunga moja na Nani alimalizia kupigilia msumari wa mwisho ktk jeneza la B'ham City.

Wednesday, May 26, 2010

Bado siku 15!


Kuanzia Juni 11 hadi July 11 mwaka huu macho ya washabiki wa mchezo unaoamika kama ndio una wapenzi wengi duniani,soka yatakuwa huko nchini Afrika ya Kusini ambako mtanange huo utakuwa ukiendelea.
Baada ya kwikwi ya muda mrefu mdau nimerejea kwa kishindo,kwahiyo wadau kaeni mkau wa kula kwa habari mbalimbali motomoto.

Thursday, February 4, 2010

NDONDI!

Floyd "Money" Mayweather Jr sasa atazipiga na mmarekani mwenzake Shane Mosley mnamo Mei mosi mwaka huu 2010 katika ukumbi wa MGM Grand huko Las Vegas California.
Mayweather na Mosley ambao waliishaanza kupigana mkwara tangu mwaka jana mara baada ya mpambano kati ya Mayweather na Juan Manuel Marquez.
Kambi za mabondia hawa wote wawili zimekubaliana na sharti ya kambi ya Mayweather la kupima damu kila wiki wakati wa maandalizi wa mpambano huo sharti ambalo lilipelekea kuvunjika kwa mpambano kati ya Mayweather na Manny Pacquiao mapema mwaka huu,kambi ya mfilipino Pacquiao ilikataa kata kata kukubaliana na sharti hilo ambalo ni staili ya michezo ya olympic.
Sasa sijui nani kati ya mabondia hawa nguli anamuhofia mwenzake?