Saturday, January 9, 2010

Barafu Nebraska..........

Leo hapa Orlando Florida tunacheza kwny nyuzi joto 36 na watu wamejifungia ndani,tulioko mitaani kwny pilika pilika za kila siku ndio tumejijaladia makoti,skafu n.k je waliko huko pande za juu kaskazini mashariki na magharibi mwa marekani kama Nebraska(pichani)wasemeje?na watoto wasiopenda shule wanaifurahia sana hali hii kwa sababu hawaendi shule lkn wanacheza kwny barafu kaaazziiii kweli kweli

Togo yajitoa michuano ya mataifa ya Africa 2010 Angola.

Golikipa wa Togo Kodjovi Obilale(kulia) aliyejeruhiwa katika shambulio la risasi kwa timu ya taifa ya Togo huko Cabinda Angola,kuna uvumi umeenea kama ameaga dunia.Mshambuliaji wa Togo Jonathan Ayite akiongea na radio ufaransa alisema Obilale amefariki,lkn kwa mujibu klabu yake ya huko ufaransa ya GSI Pontivy wanasema Obilale hajafariki.
Kodjo Samlan wa shirikisho la soka la Afrika (CAF) amethibitisha kwamba kocha msaidizi wa togo Abalo Amnalete na afisa habari Stanislas Ocloo waliojeruhiwa ktk shambulio hilo la jana wamefariki leo saa nne kamili asubuhi.Idadi ya watu waliopoteza maisha sasa imefikia watu watatu,dereva wa basi la wachezaji alifariki jana ktk eneo la tukio.
Ripoti toka ufaransa zinasema kwamba wachezaji wa togo wameamua kutoshiriki ktk michuano hiyo itayoanza hapo kesho jumapili,togo walitarajiwa kucheza na Ghana hapo jumatatu.

Friday, January 8, 2010

Patrick Vieira ajiunga na Man.City!

Patrick Vieira,33 pichani akiwa na Roberto Mancini leo mchana baada ya kusaini mkabata wa miezi sita na Man.City kukiwa na uwezekano wa kuongeza mwaka mmoja ktk mkataba wake.
Veterani Vieira aliyewahi kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya uingereza mara tatu akiwa na Arsenal,pia alishinda ligi ya Italia mara moja akiwa na Juventus na mara tatu akiwa na Inter Milan chini ya Mancini lkn alishindwa kupata namba kwny kikosi cha kwanza cha Inter chini ya Mreno Jose Maurinho.
Vieira amesema anaamini atashinda ubingwa wa uingereza kwa mara ya nne akiwa na Man.City kwa sababu bado wana nafasi na wachezaji wenye uwezo.
Wachezaji wengi barani ulaya wamekuwa wakilitumia dirisha dogo la usajili wa mwezi januari ili wapate timu ambazo watapata nafasi ya kucheza mechi nyingi kuwashawishi makocha wa timu zao za taifa kuwachagua kwa ajili ya kombe la dunia la Fifa mwaka huu huko Afrika ya Kusini.
David Beckham na Landon Donovan wote toka LA Galaxy ya hapa marekani wamejiunga kwa mkopo na Ac Milan ya Italia na Everton ya uingereza ktk kipindi hiki cha mapumziko ya ligi kuu ya soka ya marekani MLS.

Wachezaji wa Togo wavamiwa.........

Ikiwa zimesalia takriban siku mbili ili michuano ya soka ya mataifa ya Afrika ianze huko Angola,msafara wa timu ya taifa ya Togo"Sparrow Hawks"umeshambuliwa kwa risasi na waasi wanaohisiwa kuwa ni wa kikundi cha waasi wa Angola cha FLEC mara baada ya kuvuka mpaka wa Congo huko Cabinda.
Wachezaji wawili waliojeruhiwa kwa risasi ni golikipa ni Kodjovi Obilale' wa GSI Pontivy na mlinzi Serge Akakpo,22 wa Vaslui FC ya Romania ambaye ameumia vibaya na amepoteza damu nyingi lkn anaendelea vizuri baada ya matibabu,pia wengine waliojeruhiwa ni kocha msaidizi,daktari wa timu na mwandishi wa habari aliyeambatana na timu.
Waziri wa Angola anayehusika na masuala ya Cabinda Antonio Bento Bembe ameliita shambulio hilo kuwa ni la kigaidi na kukanusha kuwa sio kikundi cha waasi cha FLEC ndio kimehusika kwa sababu kundi hilo halipo tena,bali amewatuhumu watu binafsi wanaotaka kuwasababishia matatizo.
Mshambuliaji wa Emmanuel Adebayor wa Manchester City hakuumia ktk shambulio hilo,pia Moustapha Salifou wa Aston Villa zote za Uingereza naye kamuumia kwa mujibu ya tovuti za vilabu vyao.
Togo imetishia kujitoa ktk mashindano hayo makubwa barani Afrika yanayotarajiwa kuanza jumapili hii trh 10/01/2010.
Haya ni matukio ya aibu kwa bara zima la Afrika........

Wednesday, January 6, 2010

Karne ya 21 mawasiliano muhimu...

Wadau wa orlando FL, MarcJr na Imma siku ya christmass 2009.....

Tunawatakia amani na upendo 2010!

Mzee wa ng'ambo(shoto) akiwa na mdau wa orlando MarcJr(kati) na chalii wa Daytona Beach Abayu siku ya Christmas!

Friday, January 1, 2010

Wanenguaji wa Fm Academia Wazee wa Ngwasuma!

Siku ya mkesha wa mwaka mpya wazee wa ngwasuma walikuwa kijiji cha makumbusho,kwa mujibu wa wadau wa bongo naskia palikuwa hapatoshi jamaa walipiga sebene la kufa mtu!!
Nawashauri wadau wa ng'ambo siku mkitua bongo vekesheni fupi msikose kwenda kuwacheki hawa jamaa.

KHERI YA MWAKA MPYA 2010 KWA WADAU WOTE!

Mimi kama mdau mwenzenu napenda kuwatakia kheri na fanaka tele za mwaka huu mpya 2010.Ingawa hali ya uchumi duniani bado haijatengemaa lakini tusife moyo tuendelee kupambana na hali halisi ya maisha popote pale tulipo kuanzia nyumbani bongo TZ hadi ughaibuni ama ng'ambo!
Libeneke la blog kama kawa 2010 subirini mambo kibao mapya...............