Saturday, December 26, 2009

UGAIDI HADI SIKU YA CHRISTMAS!!!!!????


Raia wa Nigeria Umar Farouk Abdul Mutallab,23 anatuhumiwa kutaka kuilipua ndege ya kampuni ya Northwest Airlines huko Detroit Michigan ikitokea Amsterdam Uholanzi.
Umar mtoto wa mwenyekiti wa benki ya First Bank ya huko Nigeria Alhaji Umaru Mutallab ambaye alisema hawezi kithibitisha kama mtoto wake alikuwemo kwny ndege hiyo mpaka atakapoongea na mamlaka zinazihusika za huko Naigeria jumamosi hii,lkn anaamini mtoto wake aliwahi kwenda Yemen ambako inahisiwa ndiyo alifundishwa jinsi ya kulipua ndege.
Pongezi kwa mmoja wa abiria wa ndege hiyo kwa kuonyesha ujasiri wa kuruka viti kadhaa na kwenda kumdhibiti mtuhumiwa na hatimaye kuwekwa chini ya ulinzi mkali,alitolewa kwny ndege akiwa ameishafungwa pingu huku akiwa na majeraha ya moto miguuni mwake.
Kaazi kweli kweli,naona Wanaigeria wanaosifika kwa "utapeli"duniani sasa washaingia na kwny vitendo vya "ugaidi"...!

BOXING DAY NJEMA WADAU..........

MERRY CHRISTMAS WADAU WOTE WA BONGO NA NG'AMBO!

Friday, December 18, 2009

Ratiba ya mechi za hatua ya mtoano ya ligi ya mabwingwa wa ulaya!UEFA Champs League.

VfB STUTTGART VS BARCELONA
OLYMPIAKOS VS BORDEAUX
INTERNAZIONALE VS CHELSEA
BAYERN MUNICH VS FIORENTINA
CSKA MOSCOW VS SEVILLA FC
LYON VS REAL MADRID
FC PORTO VS ARSENAL
AC MILAN VS MANCHESTER UNITED
MECHI ZA MGUU WA KWANZA NI FEBRUARY 16&17 NA 23&24
MECHI ZA MGUU WA PILI NI MACHI 9&10 NA 16&17
Kufuatia ratiba hii iliyopangwa leo mchana huko Nyon Ufaransa,washabiki wa mchezo wa mpira wa miguu ama soka wanatarajia kushurudia David Beckham akirudi Old Trafford Manchester akiwa na jezi ya AC Milan ya Italia anayotarajia kujiunga nayo kwa mkopo mapema mwakani ili kujiweka fiti kwa ajili ya kombe la dunia 2010 huko Afrika ya Kusini endapo atateuliwa kikosini.Beckham alihamia Real Madrid mwaka 2003 akitokea Manchester.
Pia kocha wa zamani wa Chelsea Jose Maurinho atarejea Stamrod Bridge safari hii akiwa na Internazionale Milano ya Italia.Mourinho aliiongoza Chelsea kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya uingereza kwa misimu miwili mfululizo 2005 na 2006 kabla hajatumiliwa mapema msimu wa 2007/2008.
Nako Lyon Ufaransa watamkaribisha mshambuliaji wao mahiri Karim Benzema akiwa na Real Madrid.

Thursday, December 10, 2009

TIGER WOODS AAHIRISHA KUWA MPAMBE WA HARUSI YA RAFIKI YAKE.

Tiger Woods ameahirisha kuhudhuria tafrija ya harusi ya mbunifu yake itakayofanyika hivi karibuni huko South Carolina ambapo ilikuwa awe mpamba wa Bw.harusi.
Hii yote inatokana na mikasa inayoibuka kila siku kuhusu maisha ya mcheza gofu huyu nguli duniani.
Woods hajaonekana hadharani tangu apate ajali usiku wa sikukuu ya Thanksgiving.Woods ambaye huingiza takriban $ millioni 110 kutoka na matangazo mbalimbali ya biashara yuko hatarini kupoteza kipato hicho baada ya makampuni kadhaa kuonyesha njia ya kutosaini naye mikataba mingine pindi ya sasa utakapoisha,baadhi ya makampuni hayo ni Gatorade,EA Sports,Nike,ESPN n.k
Wakati huo huo hapo jana kidosho wa kwanza kuhushishwa na Woods Jamie Grubbs amemuomba msamaha Elin Woods mke wa Tiger Woods kwa kila alichikuwa akiifanyia familia yake nakudai kuwa hakujua kama Woods alikuwa ameoa!!!!!!???
Watu wa karibu wa Elin Woods walikaririwa na jarida la People wakisema kuwa Elin hatadai talaka kutokana na kujali hatma ya watoto wake wawili aliozaa na Woods.
Pia marafiki hao waliongeza kuwa Elin alijua kuwa Woods "hajatulia"kabla hawajaoana lkn aliahidi kubadilika baada ya ndoa.
Mr and Mrs Woods inasemekana wanahudhuria ushauri nasaha kuhusu ndoa.
Kila la kheri familia ya Woods,kwani ulimwengu wa mchezo wa gofu bado unahitaji mchango wa jamaa................ambaye ili kushiriki tu michuano ya gofu lazma alambe $milioni tatu....

SENETI YA FLORIDA YAPITISHA MUSWADA WA SUN RAIL KWA KURA 27 KWA 10

Seneti ya Florida ilikutana jana huko makao makuu wa State ya Florida Tallahassee nan kupitishwa muswada wa kuanzishwa wa njia ya treni toka Deland hadi Poinciana kupitia Sanford,Lake Mary,Orlando,Sand Lake,Kissimmee,Wood Words na kuishia Poinciana.
Muswada huu ulioleta mvutano kwa muda ulipita kwa "mbinde"kutokana na kupingwa kwa nguvu na baadhi ya wajumbe kwa hoja kwamba njia hii ya treni endapo itaharibiwa na ajali itakaratabiwa kwa pesa za walipa kodi.
Mradi huu unatarajiwa kukamilika mnano mwaka 2011 na utafuatiwa na mradi mwingine wa treni iendayo kasi itakayoanzia Tampa kupitia Oralndo na kuishia Miami.
Treni hii pindi itakapoanza kufanya kazi itasaidia sana ktk kusafirisha wafanyakazi na watalii ktk miji itakayopita,kwa maana kwa hali ya sasa kama ni mfanyakazi lazma uendeshe kwenda kazini,na watalii hukodi magari.Lkn mradi wa SUN RAIL ukianza mtu ataweza kusafiri kwa $ 2.5o toka kituo hadi kituo.

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel 2009 Barack Hussein Obama!

Rais wa marekani Barack Obama ambaye wiki iliyopita ametoka kuidhinisha wanajeshi 30000 kwenda vitani Afghanistan ndio mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka 2009.
Obama ambaye bado hatajitimiza mwaka tangu aingie madarakani yeye amekiri kwamba alishtushwa na kuchaguliwa kwake akiamini kuna waliofanya mengi na kustahili tuzo hiyo.
Baadhi ya wamerakani waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni pamoja na rais Theodore Roosevelt,Marshall,Jimmy Carter,pia mpigania haki wa watu weusi Dk Martin Luther King Jr.
Pia wako rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Huru Mzee Nelson Mandela,Askofu Desmond Tutu,Mama Theresa.
Mwenyekiti wa tuzo ya Nobel alisema Obama anastahili tuzo hiyo kutokana na msimamo wake kuhusu uhusiano wa kimataifa na kidiplomasia ktk kutatua matatizo kama urutubushaji wa nishati za nyuklia huko Irani na Korea ya Kaskazini,Pia uamuzi wa kulifunga gereza ya Guantanamo Cuba ambako watuhumiwa wa ugaidi wamekuwa wakishikiliwa na kuteswa bila kufikishwa mahakamani chini ya utawala wa aliyemtangulia.
Lakini washindi wa tuzo hiyo waliomtangulia kama Mama Wangari Maathai toka Kenya (2004),na Mohammed Elbaradi (2005) wote wamemuunga mkono walipohojiwa na shirika la utangazaji la uingereza (BBC).
Hapa marekani baadhi ya watu waliohojiwa wameonyesha kutokuunga mkono kutokana na hali halisi ya kiuchumi,ajira pamoja na watu kupoteza makazi yao.
Hata huko Oslo Norway kumekuwa na maandamano ya kupinga ushindi wa Bw.Obama.
Baadhi ya watu mashuhuri toka marekani walihudhuria hafla hiyo wakiwemo mcheza sinema Will Smith na mkewe Jada Pinket Smith,mwanamuziki Wyclif Jean.
Obama alikabidhiwa tuzo ya dhahabu,stashahada pamoja na $ 1.4 million ktk hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na familia ya malkia wa Norway na wasanii mbalimbali walitumbuiza.

Wednesday, December 9, 2009

Tumetoka mbali......................................

Enzi hizo Jite ilipokuwa Jite chini ya Kanali Fabian Massawe.Nilikuwa na mdau Zablon Mgonja(wa tatu toka kulia,waliosimama) na mimi nimesimama nyuma yake.
Shukrani ya picha:Maktaba ya Zablon Mgonja.

Nyuso za furaha.......kiswahili oyee


Mdau Zablon(mwenye suti) na mshauri wake wakiwa na nyuso za furaha baada ya kuwa na uhakika wa kulamba "Nondozzz"yake Uzamili ktk lugha huko chuo kikuu cha Madison,Wisconsin.
Mdau anajiaanda kurejea bongo mnamo mapema mwakani alinitonya kwamba yuko mbioni kuanzisha NGO ya kujimba vijima vya maji vijijini Tanzania,jamaa anastahili pongezi kwa sababu ni vijana wachache sana wenye moyo wa uzalendo kama yeye wa kumaliza nondoz huku "ng'ambo" na kurejea kusaidia nchi yake ya ahadi Tanzania,pongezi kwa mdau ni mfano wa kuigwa.

Hongera mdau wa Madison,Wisconsin!


Mdau Zablon Mgonja(katikati mwenye shati jeupe na tai)akizungukwa na wanafunzi wake wa lugha ya Kiswahili.Darasa hili lilikuwa la kuigwa kwa walimu wanaofundisha lugha za kigeni kikiwemo kiswahili.Nilivutiwa na kauli isemayo "Kama unafundisha kiswahili basi unafundisha kiswahili bila kutumia kiingereza,na kama unafundisha kiingereza kwa waswahili basi unafundisha kwa kiingereza bila kutumia kiswahili".
Nakumbuka kule nyumbani "bongo" baadhi wa walimu wa sekondari na hata chuoni walikuwa wakichanganya lugha hizi mbili wakifundisha.

Tuesday, December 8, 2009

Wazee wa kanisa kabla ya ibada!

Toka kushoto Charles,Mwnykt Sirbo,Andy "Ally Choki",mdau na Chris.
Taxedo zimetulia.....

Wadauzzzzz!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Wadau kibao wanadai eti tunafanana!!?je ni kweli ama...................

Nikiwa "Mji kasoro bahari" Dallas TX

Nilikutana na mdau wa New Mexico Lemmy(mwenye kapelo),mdau wa Dallas (kati),ilikuwa full shangwe...

Mama Mkwe wa Mkware Tiger Woods aruhusiwa kutoka hospitali.


Barbro Holmberg ambaye ni mama mkwe wa Tiger Woods,pia ni gavana wa Gavleborg county iliyoko mashariki ya kati ya Sweden amerehusiwa leo kutoka hospitali ya Health Central ambako alipelekwa tangu jana usiku kwa maumivu ya tumbo.Bi.Holmberg amekuwa hapa orlando kwa siku kadhaa,akiishi ktk kasri ya mkwe wake.
Ikumbukwe kuwa hii ni hospitali aliyotibiwa nguli wa mchezo wa gofu duniani (Woods)alipopata majeraha usoni alfajiri ya tarehe 27 mwezi uliopita,kutokana na ajali ya gari ambayo imezua utata mkubwa na wanahabari kutaka kujua ilisababishwa na nini?Woods mwenyewe alisema ni ajali ya kawaida na yalikuwa makosa yake ingawa redio mbao kila moja inasema lake!!!!!
Kwa upande mwingine wa sakata hili,mpaka kufikia leo idadi ya wanawake wanaodai kuwa na uhusiano wa kingono na Bw.Woods wamefikia tisa,baada ya mapema leo mwanamke mwingine wa orlando Mindy Lawton; 33 ameliambia jarida moja la uingereza "News of the World"kuwa alikuwa na uhusiano na Woods kwa takriban miaka miwili kabla mke wa Woods, Elin hajapata ujauzito wake wa kwanza.
Lawton ambaye alikuwa meneja wa mgahawa wa Perkins ulioko Conroy-Windermere karibu na kasri ya Bw.Woods iliyoko Isleworth-Windermere,alisema alikutana na Woods ktk mgahawa huo na Woods alimualika kinywaji ktk "kilabu"kingine maarufu hapa Orlando cha Blue Martini VIP ambako baada ya kinywaji Woods alimwambia kuwa ana mvuto na wakaondoka wote kwenda kwny kasri yake!
Aliongeza kuwa uhusiano wao ulidumu kwa muda mpaka Woods alipomuacha baada ya kukutana na mhudumu wa vinywaji vikali Jamie Grubbs wa huko LA ambaye ametoa ujumbe wa sauti ambao anadai ni wa Woods akimuomba aondoe jina lake ktk orodha yake ya majina kwny simu yake kwa sababu mkewe Elin ameshtukia mchongo...........

Friday, December 4, 2009

Allen Iverson arejea Philly76ers!

Allen Iverson,34 aliyewahi kucheza mechi 10 za wachezaji nyota wa NBA almaarufu kama "All Star Game"amerejea rasmi ktk timu yake ya nyumbani Philadelphia 76ers na kukabidhiwa jezi yake ya zamani namba 3 baada ya kuondoka Memphis Glizzers(kwa wakina Hasheem Thabeet)alikocheza mechi tatu tu.
Iverson alihama Sixers misimu miwili iliyopita na kuhamia Denver Nuggets na baadaye Detroit Pistons ili kukamilisha dili la Denver kumsajili Chauncey Billups lkn ktk timu hizi mbili alikuwa akitumiwa kama mchezaji wa akiba,mpaka msimu huu alipoushangaza ulimwengu wa kikapu kwa kujiunga ana Memphis timu inayoundwa na wachezaji wengi chipukizi ktk ligi ya NBA;na baadhi ya wadau wa kikapu kutabiri labda ndiyo mwisho wa Iverson.
Lkn baada ya mechi tatu alitangaza kuachana na Memphis kwa sababu zake binafsi,pia ikasemekana anafikiria kustaafu hadi wiki hii iliposemekana kuwa Sixers wamempa nafasi ya kujiunga nao tena.
Iverson (pichani)alibubujikwa na machozi wakati akitangaza rasmi kurejea Sixers na kusema bado ana mapenzi ya dhati na mashabiki wake wa Sixers na washabiki wanampenda.
Kila la kheri Iverson,washabiki wa mchezo wa kikapu hususan wa Sixers wanaamini bado una uwezo wa kuisadia timu yako.

2010 FIFA WORLD CUP GROUPS,SOUTH AFRICA.

Group A: South Africa,Mexico,Uruguay,France.

B: Argentina,South Korea,Nigeria,Greece.

C: England,U.S.A,Algeria,Slovenia.

D: Germany,Australia,Serbia,Ghana.

E: Holland,Denmark,Japan,Cameroon.

F: Italy,Paraguay,New Zealand,Slovakia.

G: Brazil,North Korea,Cote D'ivore,Portugal.

H: Spain,Switzerland,Honduras,Chile.

Wadau wa soka haya makundi ni vipi!?timu za Afrika zitaweza kusonga mbele kweli kwa mtaji huu?hivi tuna gundu ama ni fitna za Fifa hebu angalieni kundi "G" hawa jamaa wanatutakia mema kweli!??kuna haja ya kujiimarisha zaidi ktk viwango vya ubora wa soka duniani ili kuepuka kukutana na timu kubwa ktk hatua ya awali ya makundi,kwa maana hapo ni timu mbili tu ndio zinazotakiwa kusonga mbele ktk hatua ya mtoano,lkn poa tutasonga tu mungu yupo.......tutakomaa nao

Wednesday, December 2, 2009

Matukio mbalimbali ya siku mdau wa dallas TX alipoji-commit rasmi,tunawatakia kila la kheri ktk maisha mapya ya ndoa!
















Nilikutana na wadau Joe Dakota(t-shirt ya njano) na Obedi(black tshirt)baada ya miaka kibao...
















My son wangu Marc Mark na back pack yake sijui alibeba nini!?

Mdau wa Orlando akinyoosha miguu baada ya kuchimba dawa Louisiana jirani na mpaka wa Texas.....hii ilikuwa ndio safari yake ya kwanza nje ya Florida.

Tukivuka mto Mississippi,nilifurahi kuuona baada ya kuusoma sana kwny Jeografia shule ya msingi na sekondari..tembea uone


Ndani ya tunnel Mobile-Alabama,huku ng'ambo nimewavulia kofia kwa miundombinu kama hii lol


Safari ya kutoka orlando FL kwenda dallas TX ilianza kama utani vile,lkn mashine ilipigwa kwa masaa 17,mapumziko petrol station kuweka "wese"


FIFA kumchunguza Thierry Henry.

Rais wa Fifa Sepp Blatter amesema kamati ya nidhamu ya Fifa itakutana baadaye mwezi huu kuchunguza tukio la mshambuliaji wa ufaransa Henry kushika mpira ktk mechi ya mtoano ya kufuzu kushiriki kombe la dunia la mwakani huko south africa.Lkn Blatter hakusema kwamba henry anaweza kukumbana na adhabu ya kufungiwa,pia Fifa imelitakaa pendekezo wa kutaka waongezwe waamuzi wawili watakaosimaa nyuma ya mstari wa goli ili kukabiliana na wachezaji wadanganyifu kama henry,pia wamepingana na pendekezo jingine la matumizi ya teknolojia ya televisheni kupata ukweli.
Hii ina maana kwamba ktk kombe la dunia la mwakani hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya kanuni za mchezo wa soka.
Blatter aliongeza kuwa hata yeye ktk kipindi chake cha uchezaji ambapo alikuwa mshambuliaji namba tisa alikuwa akitumia mikono yake kumsukuma beki ili aweze kufunga lkn sio kushika mpira!
Kila la kheri kwa waamuzi wa kombe la dunia,mtaendelea kubeba lawama kutokana na wachezaji wadanganyifu waojiangusha kwny penati box ili wapewe penati za za bure!

Tiger Woods Saga is Over!

Woods amepigwa faini ya $ 164 ama paundi 99 na pointi 4 ktk leseni yake kwa kosa la kuendesha gari kizembe na kugonga mti na bomba kubwa la maji kwa ajili ya dharura kama moto.Florida Highway Patrol ktk ripoti yao waliyoitoa jana mchana walisema kwamba kesi amekwisha na hakuna uchunguzi wowote utakaondelea,pia Woods hatakabiliana na adhabu ya makosa ya jinai.
Woods imebidi ajitoe kwny michuano ya California Open iliyoanza jana kutokana na sakata hili lililotokea ijumaa alfajiri baada ya sikukuu ya Thanksgiving.
Leo asubuhi Woods ametoa taarifa yake fupi kuwa ameiangusha familia yake kutokana na tabia yake na ameomba radhi,atalimaliza suala hili ndani ya familia yake.
Kumekuwa tetesi kuwa Woods amekuwa na uhusiano usiofaa na vidosho wawili wa huko LA California ingawa mmoja wao amekanusha leo hii kwamba yeye na Woods ni marafiki tu na waliwahi kuonana mara mbili tu,lkn kidosho mwingine anadai alikuwa na uhusiano wa kingono na ana msg pamoja na ujumbe wa sauti toka kwa nguli huyo wa mchezo wa golf duniani.
Woods ambaye anaishi kwny kitongoji cha watu wenye nazo hapa Orlando,FL Isleworth Windermere-Orange County,mmoja wa majirani zake ndio alipiga 911 baada ya Woods kugonga mti.
Duh kweli umaarufu una mambo,maana tangu mkasa huu utokee karibu kila redio mbao inasema lake,sijui eti alikuwa akigombana na mkewe ndio mkewe akavunja kioo cha SUV ya jamaa na tayari kwny mtandao kuna wajanja wameishatengeneza vikaragosi vya mkasa huo jinsi ulivyokuwa yaani kama walikuwepo vile.............mmmhh

Sunday, November 29, 2009

Kumradhi wadau siko hewani tangu juzi niko safarini,kwny mnuso na kiji-vekesheni kidogo cha thanksgiving hapa mji kasoro bahari dallas texas,kwhy msikonde wadau kaeni mkao wa kula subirini taswiraz za kumwaga.........................................

Monday, November 23, 2009

BWI tayari kurudisha mkoko wa kukodi kabla ya kukwea gari moshi kuelekea Philly,PA kumalizia vekesheni yangu ya bila malipo duh!


Club Safari with my primary school mate Rich,naye tulikuwa hatujaonana tangu tumalize elimu ya msingi enzi zileee,kumbe alitimkia "ng'ambo"


Kweli milima haikutani lkn binadamu hukutana,baada ya takriban muongo mmoja nilikutana na mdau John6(mbele)aliyejichimbia huko kwa Obama!


Nikila "mikonozzz" na my uncle,aunt na mdau wa TX,kwa Obama jumba jeupe!


Club Ozio nikiwa na wadau wa Dc Jenge & Jabir,hii club ina ghorofa kama tano hivi zinazopita muziki wa mahadhi tofauti,hapa anakamua m-bongo DJ Joe!


Mzee wa ng'ambo akiwa vekesheni fupi kwa Obama,uncle GK,mdau wa Texas mtembelee ktk (willemwamba.blogspot.com) na mdau wa Dc Jabir.Club Safari DC.


Mzee wa ng'ambo akiwa kwny mnuso wa kuzaliwa wa mdau Jimmy K(mwenye T-shirt nyekundu),DJ Evy na mdau wa Kibaigwa Joram aliyeshika beer.


Friday, November 20, 2009

Sakata la Ireland vs France!

Baada ya hapo jana shirikisho la soka la Ireland kuwasilisha rufani yao kwa Fifa kuomba mechi ya mtoano ya kufuzu kushiriki kombe la dunia 2010 huko Afrika ya Kusini irudiwe,leo Fifa imetoa majibu ambapo imekataa rufaa hiyo na kusisitiza kwamba kanuni namba tano ya shirikisho hilo isemayo uamuzi wa refa ni wa mwisho,ingawa Thierry Henry mwenyewe amekiri kwamba aliunawa mpira kwa makusudi!!!!Kweli umefika wakati wa Fifa kuruhusu matumizi ya teknolojia ya picha za televisheni kutatua matatizo kama haya ya wachezaji wadanganyifu.
Pole kwa kocha,wachezaji,mashabiki wa soka wa Ireland,timu mnayo na ilistahili kukata tiketi ya kwenda Afrika ya Kusini.