Baada ya hapo jana shirikisho la soka la Ireland kuwasilisha rufani yao kwa Fifa kuomba mechi ya mtoano ya kufuzu kushiriki kombe la dunia 2010 huko Afrika ya Kusini irudiwe,leo Fifa imetoa majibu ambapo imekataa rufaa hiyo na kusisitiza kwamba kanuni namba tano ya shirikisho hilo isemayo uamuzi wa refa ni wa mwisho,ingawa Thierry Henry mwenyewe amekiri kwamba aliunawa mpira kwa makusudi!!!!Kweli umefika wakati wa Fifa kuruhusu matumizi ya teknolojia ya picha za televisheni kutatua matatizo kama haya ya wachezaji wadanganyifu.
Pole kwa kocha,wachezaji,mashabiki wa soka wa Ireland,timu mnayo na ilistahili kukata tiketi ya kwenda Afrika ya Kusini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment