Saturday, January 9, 2010

Togo yajitoa michuano ya mataifa ya Africa 2010 Angola.

Golikipa wa Togo Kodjovi Obilale(kulia) aliyejeruhiwa katika shambulio la risasi kwa timu ya taifa ya Togo huko Cabinda Angola,kuna uvumi umeenea kama ameaga dunia.Mshambuliaji wa Togo Jonathan Ayite akiongea na radio ufaransa alisema Obilale amefariki,lkn kwa mujibu klabu yake ya huko ufaransa ya GSI Pontivy wanasema Obilale hajafariki.
Kodjo Samlan wa shirikisho la soka la Afrika (CAF) amethibitisha kwamba kocha msaidizi wa togo Abalo Amnalete na afisa habari Stanislas Ocloo waliojeruhiwa ktk shambulio hilo la jana wamefariki leo saa nne kamili asubuhi.Idadi ya watu waliopoteza maisha sasa imefikia watu watatu,dereva wa basi la wachezaji alifariki jana ktk eneo la tukio.
Ripoti toka ufaransa zinasema kwamba wachezaji wa togo wameamua kutoshiriki ktk michuano hiyo itayoanza hapo kesho jumapili,togo walitarajiwa kucheza na Ghana hapo jumatatu.

No comments:

Post a Comment