
Veterani Vieira aliyewahi kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya uingereza mara tatu akiwa na Arsenal,pia alishinda ligi ya Italia mara moja akiwa na Juventus na mara tatu akiwa na Inter Milan chini ya Mancini lkn alishindwa kupata namba kwny kikosi cha kwanza cha Inter chini ya Mreno Jose Maurinho.
Vieira amesema anaamini atashinda ubingwa wa uingereza kwa mara ya nne akiwa na Man.City kwa sababu bado wana nafasi na wachezaji wenye uwezo.
Wachezaji wengi barani ulaya wamekuwa wakilitumia dirisha dogo la usajili wa mwezi januari ili wapate timu ambazo watapata nafasi ya kucheza mechi nyingi kuwashawishi makocha wa timu zao za taifa kuwachagua kwa ajili ya kombe la dunia la Fifa mwaka huu huko Afrika ya Kusini.
David Beckham na Landon Donovan wote toka LA Galaxy ya hapa marekani wamejiunga kwa mkopo na Ac Milan ya Italia na Everton ya uingereza ktk kipindi hiki cha mapumziko ya ligi kuu ya soka ya marekani MLS.
No comments:
Post a Comment