
Raia wa Nigeria Umar Farouk Abdul Mutallab,23 anatuhumiwa kutaka kuilipua ndege ya kampuni ya Northwest Airlines huko Detroit Michigan ikitokea Amsterdam Uholanzi.
Umar mtoto wa mwenyekiti wa benki ya First Bank ya huko Nigeria Alhaji Umaru Mutallab ambaye alisema hawezi kithibitisha kama mtoto wake alikuwemo kwny ndege hiyo mpaka atakapoongea na mamlaka zinazihusika za huko Naigeria jumamosi hii,lkn anaamini mtoto wake aliwahi kwenda Yemen ambako inahisiwa ndiyo alifundishwa jinsi ya kulipua ndege.
Pongezi kwa mmoja wa abiria wa ndege hiyo kwa kuonyesha ujasiri wa kuruka viti kadhaa na kwenda kumdhibiti mtuhumiwa na hatimaye kuwekwa chini ya ulinzi mkali,alitolewa kwny ndege akiwa ameishafungwa pingu huku akiwa na majeraha ya moto miguuni mwake.
Kaazi kweli kweli,naona Wanaigeria wanaosifika kwa "utapeli"duniani sasa washaingia na kwny vitendo vya "ugaidi"...!