Friday, December 4, 2009

Allen Iverson arejea Philly76ers!

Allen Iverson,34 aliyewahi kucheza mechi 10 za wachezaji nyota wa NBA almaarufu kama "All Star Game"amerejea rasmi ktk timu yake ya nyumbani Philadelphia 76ers na kukabidhiwa jezi yake ya zamani namba 3 baada ya kuondoka Memphis Glizzers(kwa wakina Hasheem Thabeet)alikocheza mechi tatu tu.
Iverson alihama Sixers misimu miwili iliyopita na kuhamia Denver Nuggets na baadaye Detroit Pistons ili kukamilisha dili la Denver kumsajili Chauncey Billups lkn ktk timu hizi mbili alikuwa akitumiwa kama mchezaji wa akiba,mpaka msimu huu alipoushangaza ulimwengu wa kikapu kwa kujiunga ana Memphis timu inayoundwa na wachezaji wengi chipukizi ktk ligi ya NBA;na baadhi ya wadau wa kikapu kutabiri labda ndiyo mwisho wa Iverson.
Lkn baada ya mechi tatu alitangaza kuachana na Memphis kwa sababu zake binafsi,pia ikasemekana anafikiria kustaafu hadi wiki hii iliposemekana kuwa Sixers wamempa nafasi ya kujiunga nao tena.
Iverson (pichani)alibubujikwa na machozi wakati akitangaza rasmi kurejea Sixers na kusema bado ana mapenzi ya dhati na mashabiki wake wa Sixers na washabiki wanampenda.
Kila la kheri Iverson,washabiki wa mchezo wa kikapu hususan wa Sixers wanaamini bado una uwezo wa kuisadia timu yako.

No comments:

Post a Comment