Seneti ya Florida ilikutana jana huko makao makuu wa State ya Florida Tallahassee nan kupitishwa muswada wa kuanzishwa wa njia ya treni toka Deland hadi Poinciana kupitia Sanford,Lake Mary,Orlando,Sand Lake,Kissimmee,Wood Words na kuishia Poinciana.
Muswada huu ulioleta mvutano kwa muda ulipita kwa "mbinde"kutokana na kupingwa kwa nguvu na baadhi ya wajumbe kwa hoja kwamba njia hii ya treni endapo itaharibiwa na ajali itakaratabiwa kwa pesa za walipa kodi.
Mradi huu unatarajiwa kukamilika mnano mwaka 2011 na utafuatiwa na mradi mwingine wa treni iendayo kasi itakayoanzia Tampa kupitia Oralndo na kuishia Miami.
Treni hii pindi itakapoanza kufanya kazi itasaidia sana ktk kusafirisha wafanyakazi na watalii ktk miji itakayopita,kwa maana kwa hali ya sasa kama ni mfanyakazi lazma uendeshe kwenda kazini,na watalii hukodi magari.Lkn mradi wa SUN RAIL ukianza mtu ataweza kusafiri kwa $ 2.5o toka kituo hadi kituo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment