Wednesday, December 2, 2009

FIFA kumchunguza Thierry Henry.

Rais wa Fifa Sepp Blatter amesema kamati ya nidhamu ya Fifa itakutana baadaye mwezi huu kuchunguza tukio la mshambuliaji wa ufaransa Henry kushika mpira ktk mechi ya mtoano ya kufuzu kushiriki kombe la dunia la mwakani huko south africa.Lkn Blatter hakusema kwamba henry anaweza kukumbana na adhabu ya kufungiwa,pia Fifa imelitakaa pendekezo wa kutaka waongezwe waamuzi wawili watakaosimaa nyuma ya mstari wa goli ili kukabiliana na wachezaji wadanganyifu kama henry,pia wamepingana na pendekezo jingine la matumizi ya teknolojia ya televisheni kupata ukweli.
Hii ina maana kwamba ktk kombe la dunia la mwakani hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya kanuni za mchezo wa soka.
Blatter aliongeza kuwa hata yeye ktk kipindi chake cha uchezaji ambapo alikuwa mshambuliaji namba tisa alikuwa akitumia mikono yake kumsukuma beki ili aweze kufunga lkn sio kushika mpira!
Kila la kheri kwa waamuzi wa kombe la dunia,mtaendelea kubeba lawama kutokana na wachezaji wadanganyifu waojiangusha kwny penati box ili wapewe penati za za bure!

No comments:

Post a Comment