
Barbro Holmberg ambaye ni mama mkwe wa Tiger Woods,pia ni gavana wa Gavleborg county iliyoko mashariki ya kati ya Sweden amerehusiwa leo kutoka hospitali ya Health Central ambako alipelekwa tangu jana usiku kwa maumivu ya tumbo.Bi.Holmberg amekuwa hapa orlando kwa siku kadhaa,akiishi ktk kasri ya mkwe wake.
Ikumbukwe kuwa hii ni hospitali aliyotibiwa nguli wa mchezo wa gofu duniani (Woods)alipopata majeraha usoni alfajiri ya tarehe 27 mwezi uliopita,kutokana na ajali ya gari ambayo imezua utata mkubwa na wanahabari kutaka kujua ilisababishwa na nini?Woods mwenyewe alisema ni ajali ya kawaida na yalikuwa makosa yake ingawa redio mbao kila moja inasema lake!!!!!
Kwa upande mwingine wa sakata hili,mpaka kufikia leo idadi ya wanawake wanaodai kuwa na uhusiano wa kingono na Bw.Woods wamefikia tisa,baada ya mapema leo mwanamke mwingine wa orlando Mindy Lawton; 33 ameliambia jarida moja la uingereza "News of the World"kuwa alikuwa na uhusiano na Woods kwa takriban miaka miwili kabla mke wa Woods, Elin hajapata ujauzito wake wa kwanza.
Lawton ambaye alikuwa meneja wa mgahawa wa Perkins ulioko Conroy-Windermere karibu na kasri ya Bw.Woods iliyoko Isleworth-Windermere,alisema alikutana na Woods ktk mgahawa huo na Woods alimualika kinywaji ktk "kilabu"kingine maarufu hapa Orlando cha Blue Martini VIP ambako baada ya kinywaji Woods alimwambia kuwa ana mvuto na wakaondoka wote kwenda kwny kasri yake!
Aliongeza kuwa uhusiano wao ulidumu kwa muda mpaka Woods alipomuacha baada ya kukutana na mhudumu wa vinywaji vikali Jamie Grubbs wa huko LA ambaye ametoa ujumbe wa sauti ambao anadai ni wa Woods akimuomba aondoe jina lake ktk orodha yake ya majina kwny simu yake kwa sababu mkewe Elin ameshtukia mchongo...........
No comments:
Post a Comment