Thursday, December 10, 2009

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel 2009 Barack Hussein Obama!

Rais wa marekani Barack Obama ambaye wiki iliyopita ametoka kuidhinisha wanajeshi 30000 kwenda vitani Afghanistan ndio mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka 2009.
Obama ambaye bado hatajitimiza mwaka tangu aingie madarakani yeye amekiri kwamba alishtushwa na kuchaguliwa kwake akiamini kuna waliofanya mengi na kustahili tuzo hiyo.
Baadhi ya wamerakani waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni pamoja na rais Theodore Roosevelt,Marshall,Jimmy Carter,pia mpigania haki wa watu weusi Dk Martin Luther King Jr.
Pia wako rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Huru Mzee Nelson Mandela,Askofu Desmond Tutu,Mama Theresa.
Mwenyekiti wa tuzo ya Nobel alisema Obama anastahili tuzo hiyo kutokana na msimamo wake kuhusu uhusiano wa kimataifa na kidiplomasia ktk kutatua matatizo kama urutubushaji wa nishati za nyuklia huko Irani na Korea ya Kaskazini,Pia uamuzi wa kulifunga gereza ya Guantanamo Cuba ambako watuhumiwa wa ugaidi wamekuwa wakishikiliwa na kuteswa bila kufikishwa mahakamani chini ya utawala wa aliyemtangulia.
Lakini washindi wa tuzo hiyo waliomtangulia kama Mama Wangari Maathai toka Kenya (2004),na Mohammed Elbaradi (2005) wote wamemuunga mkono walipohojiwa na shirika la utangazaji la uingereza (BBC).
Hapa marekani baadhi ya watu waliohojiwa wameonyesha kutokuunga mkono kutokana na hali halisi ya kiuchumi,ajira pamoja na watu kupoteza makazi yao.
Hata huko Oslo Norway kumekuwa na maandamano ya kupinga ushindi wa Bw.Obama.
Baadhi ya watu mashuhuri toka marekani walihudhuria hafla hiyo wakiwemo mcheza sinema Will Smith na mkewe Jada Pinket Smith,mwanamuziki Wyclif Jean.
Obama alikabidhiwa tuzo ya dhahabu,stashahada pamoja na $ 1.4 million ktk hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na familia ya malkia wa Norway na wasanii mbalimbali walitumbuiza.

No comments:

Post a Comment