Wednesday, December 2, 2009

Tiger Woods Saga is Over!

Woods amepigwa faini ya $ 164 ama paundi 99 na pointi 4 ktk leseni yake kwa kosa la kuendesha gari kizembe na kugonga mti na bomba kubwa la maji kwa ajili ya dharura kama moto.Florida Highway Patrol ktk ripoti yao waliyoitoa jana mchana walisema kwamba kesi amekwisha na hakuna uchunguzi wowote utakaondelea,pia Woods hatakabiliana na adhabu ya makosa ya jinai.
Woods imebidi ajitoe kwny michuano ya California Open iliyoanza jana kutokana na sakata hili lililotokea ijumaa alfajiri baada ya sikukuu ya Thanksgiving.
Leo asubuhi Woods ametoa taarifa yake fupi kuwa ameiangusha familia yake kutokana na tabia yake na ameomba radhi,atalimaliza suala hili ndani ya familia yake.
Kumekuwa tetesi kuwa Woods amekuwa na uhusiano usiofaa na vidosho wawili wa huko LA California ingawa mmoja wao amekanusha leo hii kwamba yeye na Woods ni marafiki tu na waliwahi kuonana mara mbili tu,lkn kidosho mwingine anadai alikuwa na uhusiano wa kingono na ana msg pamoja na ujumbe wa sauti toka kwa nguli huyo wa mchezo wa golf duniani.
Woods ambaye anaishi kwny kitongoji cha watu wenye nazo hapa Orlando,FL Isleworth Windermere-Orange County,mmoja wa majirani zake ndio alipiga 911 baada ya Woods kugonga mti.
Duh kweli umaarufu una mambo,maana tangu mkasa huu utokee karibu kila redio mbao inasema lake,sijui eti alikuwa akigombana na mkewe ndio mkewe akavunja kioo cha SUV ya jamaa na tayari kwny mtandao kuna wajanja wameishatengeneza vikaragosi vya mkasa huo jinsi ulivyokuwa yaani kama walikuwepo vile.............mmmhh

No comments:

Post a Comment