Thursday, December 10, 2009

TIGER WOODS AAHIRISHA KUWA MPAMBE WA HARUSI YA RAFIKI YAKE.

Tiger Woods ameahirisha kuhudhuria tafrija ya harusi ya mbunifu yake itakayofanyika hivi karibuni huko South Carolina ambapo ilikuwa awe mpamba wa Bw.harusi.
Hii yote inatokana na mikasa inayoibuka kila siku kuhusu maisha ya mcheza gofu huyu nguli duniani.
Woods hajaonekana hadharani tangu apate ajali usiku wa sikukuu ya Thanksgiving.Woods ambaye huingiza takriban $ millioni 110 kutoka na matangazo mbalimbali ya biashara yuko hatarini kupoteza kipato hicho baada ya makampuni kadhaa kuonyesha njia ya kutosaini naye mikataba mingine pindi ya sasa utakapoisha,baadhi ya makampuni hayo ni Gatorade,EA Sports,Nike,ESPN n.k
Wakati huo huo hapo jana kidosho wa kwanza kuhushishwa na Woods Jamie Grubbs amemuomba msamaha Elin Woods mke wa Tiger Woods kwa kila alichikuwa akiifanyia familia yake nakudai kuwa hakujua kama Woods alikuwa ameoa!!!!!!???
Watu wa karibu wa Elin Woods walikaririwa na jarida la People wakisema kuwa Elin hatadai talaka kutokana na kujali hatma ya watoto wake wawili aliozaa na Woods.
Pia marafiki hao waliongeza kuwa Elin alijua kuwa Woods "hajatulia"kabla hawajaoana lkn aliahidi kubadilika baada ya ndoa.
Mr and Mrs Woods inasemekana wanahudhuria ushauri nasaha kuhusu ndoa.
Kila la kheri familia ya Woods,kwani ulimwengu wa mchezo wa gofu bado unahitaji mchango wa jamaa................ambaye ili kushiriki tu michuano ya gofu lazma alambe $milioni tatu....

No comments:

Post a Comment