Friday, December 18, 2009

Ratiba ya mechi za hatua ya mtoano ya ligi ya mabwingwa wa ulaya!UEFA Champs League.

VfB STUTTGART VS BARCELONA
OLYMPIAKOS VS BORDEAUX
INTERNAZIONALE VS CHELSEA
BAYERN MUNICH VS FIORENTINA
CSKA MOSCOW VS SEVILLA FC
LYON VS REAL MADRID
FC PORTO VS ARSENAL
AC MILAN VS MANCHESTER UNITED
MECHI ZA MGUU WA KWANZA NI FEBRUARY 16&17 NA 23&24
MECHI ZA MGUU WA PILI NI MACHI 9&10 NA 16&17
Kufuatia ratiba hii iliyopangwa leo mchana huko Nyon Ufaransa,washabiki wa mchezo wa mpira wa miguu ama soka wanatarajia kushurudia David Beckham akirudi Old Trafford Manchester akiwa na jezi ya AC Milan ya Italia anayotarajia kujiunga nayo kwa mkopo mapema mwakani ili kujiweka fiti kwa ajili ya kombe la dunia 2010 huko Afrika ya Kusini endapo atateuliwa kikosini.Beckham alihamia Real Madrid mwaka 2003 akitokea Manchester.
Pia kocha wa zamani wa Chelsea Jose Maurinho atarejea Stamrod Bridge safari hii akiwa na Internazionale Milano ya Italia.Mourinho aliiongoza Chelsea kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya uingereza kwa misimu miwili mfululizo 2005 na 2006 kabla hajatumiliwa mapema msimu wa 2007/2008.
Nako Lyon Ufaransa watamkaribisha mshambuliaji wao mahiri Karim Benzema akiwa na Real Madrid.

No comments:

Post a Comment